Kaimu Mkurugenzi wa TPHPA Prof Joseph Ndunguru atuma ujumbe wa Wataalamu wa TPHPA na AVRDC

Pichani: Kulia Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru akisalimiana na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika ya World Vegetable Centre Ndg. Gabriel Rugalema Na Innocent Natai Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru amewataka wataalamu wa mamlaka hiyo kushiriki kikamilifu katika utekelezaji ya makubaliano ya mashirikiano na kituo cha Africa World Vegetable Center (AVRDC) ili kuhakikisha nasaba za mimea zinakusanywa na kuhifadhiwa kwa wingi. Prof. Ndunguru ameyasema hayo leo March 7,2023 baada ya kufanya ziara ya kutembelea ofisi za kituo hicho kinachojihusisha na utafiti,ukusanyaji na uboreshaji wa nasaba za mbegu za mboga mboga kilichopo Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha. Aidha alisema kuwa katika mazungumzo waliyofanya wameweka makubaliano ya kushirikiana katika maeneo matatu na miongoni mwa makubaliano hayo ikiwa ni pamoja na kukusanya zaidi nasaba ka...