MATUMIZI YASIYOFAA NA UUZAJI WA VIUATILIFU BANDIA NI KIKWAZO KATIKA KUKABILIANA NA WADUDU WAHARIBIFU WA MIMIEA- TPHPA

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania, (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru Tanzania ,akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 1,2023 jijini Dodoma katika ukumbi wa Idara ya Habari, wakati akielezea majukumu na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo.



Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania, (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru, akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 1,2023 jijini Dodoma, wakati akielezea majukumu na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo.

Na Innocent Natai

Matumizi yasiyosahihi ya viuatilifu na udaganyifu wa baadhii ya wauzaji wa viuatilifu na mazao ya mimea imekuwa kikwazo katika kukabiliana na wadudu waharibifu wa mimea nchini.


Hayo yameelezwa jijini Dodoma leo Machi 1,2023 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru wakati akielezea majukumu na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo.

Prof.Ndunguru amesema kuwa Uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, na uwepo wa wauzaji wa Viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu imesababisha kuendelea kuwepo kwa wadudu visumbufu wa mimea.

“Matumizi yasiyosahihi ya viuatilifu na udaganyifu wa baadhii ya wauzaji wa viuatilifu changanya na Uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, na uwepo wa wauzaji wa Viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu imesababisha kuendelea kuwepo kwa wadudu visumbufu wa mimea,”amesema Prof.Ndunguru

Aidha Prof.Ndunguru, ameeleza madhara ya kutumia viuatilifu visivyo sahihi kwa wakulima kuwa inawaongezea gharama kwa sababu mkulima analazimika kutumia viuatilifu vingi  na inaathiri afya yake na mazingira kwa ujumla.

“Madhara ni mengi ndio maana tulitilia mkazo kwa kuwajengea uelewe wakulima juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu sababu wanapopulizia viuatilifu visivyosahihi vinawajengea usugu wadudu waharibifu na kuuwa wadudu rafiki wa mimea,” amesema Prof.Ndunguru

Akitoa takwimu za Uchambuzi wa sampuli mbalimbali zilizofanywa na  Mamlaka hiyo ,Prof.Ndunguru ameeleza kuwa sampuli 1025 za viuatilifu (analysis of pesticide samples) ambazo zimeshafanyika ikiwa sampuli 1005 sawa na asilimia (98.04%) zilikidhi viwango huku sampuli 20 (1.96%) zimeonesha kutokidhi viwango.

Na kusema kuwa Jumla ya viuatilifu vipya 409 na kampuni za ufukizaji
198 vilisajiiliwa huku Vibali vya shehena za viuatilifu 1324 vyenye ujazo wa lita 58,379,97.98 na kilogram 3,880,772.77 ambapo Jumla ya vibali vya maduka 802 vilitolewa kwa wafanyabiashara wa Viuatilifu.

''Jumla ya viuatilifu vipya 409 na kampuni za ufukizaji 198 vilisajiiliwa Vibali vya shehena za viuatilifu 1324; ujazo wa lita 58,379,97.98 na kilogram 3,880,772.77 Mapato kiasi cha TZS Bilioni 3.06 Jumla ya vibali vya maduka 802 vilitolewa kwa wafanyabiashara wa Viuatilifu''Amesema Ndunguru.

Aidha amesema Mamlaka kwa kushirikiana na Wizara ya kilimo imefanya uchambuzi wa sampuli za udongo takribani 1300 kutoka kwenye mashamba ya “Block farming”na kutumia Matokeo ya uchambuzi yatawezesha kutoa ushauri kulingana na eneo husika.

Majukumu ya mamlaka ya afya ya mimea na viuatilifu ni Kuwezesha biashara ya mimea na mazao ya mimea hapa nchini na kimataifa Pamoja na Kudhibiti uagizaji, usafirishaji, utengenezaji, usambazaji, uuzaji, matumizi ya viuatilifu na vifaa vya unyunyiziaji wa viuatilifu.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu