TPHPA yafika Zanzibar kudhibiti wa Panya Waharibifu//Waziri wa Kilimo na Katibu Mkuu wawamwagia Sifa

Na Innocent Natai - Zanzibar Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Khamis ameitaka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Kuona namna ya kuanzisha ofisi ndogo katika visiwa hivyo ili kutoa huduma za udhibiti wa visumbufu vya Mimea kwa haraka ili kunusuru upotevu wa Mazao kabla na baada ya mavuno kwani huduma za Mamlaka hiyo pia zinahitajika Zanzibar Ameyasema hayo Mei 15,2024 katika Kijiji cha Cheju, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar wakati akifungua oparesheni ya kudhibiti panya Waharibifu wa Mazao waliovamia katika mabonde nane ya umwagiliaji kwa upande Wa Unguja na Pemba yenye jumla ya Hekta 514.6 zoezi lililo hudhuriwa na Wataalamu na Viongozi kutoka Wizara hiyo Zanzibar, Wataalamu kutoka TPHPA na mamia ya Wakulima Aidha Mhe. Shamata ameipongeza Mamlaka kwa utendaji wake wa kazi hasa kwenye udhibiti wa visumbufu vya mimea na kusema kuwa kwa Zanzibar wamekuwa wakisumbuliwa na inzi wa matunda na sasa panya waharibi...