TPHPA yafika Zanzibar kudhibiti wa Panya Waharibifu//Waziri wa Kilimo na Katibu Mkuu wawamwagia Sifa
Na Innocent Natai - Zanzibar
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Mhe. Shamata Khamis ameitaka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Kuona namna ya kuanzisha ofisi ndogo katika visiwa hivyo ili kutoa huduma za udhibiti wa visumbufu vya Mimea kwa haraka ili kunusuru upotevu wa Mazao kabla na baada ya mavuno kwani huduma za Mamlaka hiyo pia zinahitajika Zanzibar
Ameyasema hayo Mei 15,2024 katika Kijiji cha Cheju, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar wakati akifungua oparesheni ya kudhibiti panya Waharibifu wa Mazao waliovamia katika mabonde nane ya umwagiliaji kwa upande Wa Unguja na Pemba yenye jumla ya Hekta 514.6 zoezi lililo hudhuriwa na Wataalamu na Viongozi kutoka Wizara hiyo Zanzibar, Wataalamu kutoka TPHPA na mamia ya Wakulima
Aidha Mhe. Shamata ameipongeza Mamlaka kwa utendaji wake wa kazi hasa kwenye udhibiti wa visumbufu vya mimea na kusema kuwa kwa Zanzibar wamekuwa wakisumbuliwa na inzi wa matunda na sasa panya waharibifu wamevamia katika mashamba ya Mpunga hivyo jitihada za Mamlaka hiyo zinahitajika kwa ukaribu wakishirikiana na wataalamu wa Wizara hiyo
“katika janga hili nimeona Wizara imekaa mstari wa mbele lakini pia na hawa wenzetu TPHPA kutoka Tanzania bara tumeonesha utayari wa pamoja na umahiri wa kupambana na panya hawa hayo ni matunda ya Muungano wetu ni wapongezeni sana” alisema Mhe. Shamata
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar Ndg. Ali Khamis Juma ameipongeza Mamlaka kwa kazi inazozifanya za kusaidia wakulima huku akipongeza zaidi uharaka wa kutatua changamoto kabla hazijaleta madhara makubwa
” Tumewatumia barua hata haujapiata muda wametujibu na sasa wamekuja kwa haraka hili ni Jambo la kuigwa hapa wameonesha ni jinsi gani hawana urasimu” alidokeza Ndg. Ali Juma
Akizungumza Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Dkt. Mahamudu Sasamalo ambaye ni Kaimu Meneja TPHPA Kanda ya Mashariki amesema kuwa Mamlaka kupitia Kituo chake Cha Udhibiti wa Baa la Panya Kilichopo Morogoro imekuwa ikisaidia Wakulima kuwadhibiti panya hao waharibifu katika maeneo mbalimbali Tanzania bara na sasa wamefika kufanya zoezi hilo Zanzibar
Ameongeza kuwa Panya ni viumbe hatari kwa mustakabali wa chakula kwani wakivamia katika mashamba au maghala wanaweza kuharibu kwa asilimia Mia moja ya mazao na kusababisha baa la njaa hivyo amewataka viongozi hao kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya Wizara ya Kilimo Tanzania Bara na Zanzibar ili kutoa huduma hiyo kwa haraka kwa wakulima
Comments
Post a Comment