Posts

Showing posts from January, 2025

WASAFIRISHAJI WA MAZAO WAHIMIZWA KUTUMIA BANDARI YA TANGA,WAHAKIKISHIWA KUWEPO HUDUMA BORA ZA UKAGUZI KUTOKA TPHPA

Image
Hayo yamesemwa na Kaimu Afisa  Mfawidhi wa Kituo cha TPHPA kilichopo Bandari ya Tanga Bi Monica Sylvester Kuziwa ambapo amewataka Wasafirishaji wa mazao  nchini kuwa wazalendo na kutumia Bandari ya Tanga kusafirisha mazao yao  na kupata huduma bora za ukaguzi wa mazao hayo inayotelewa na Ofisi ya Kituo cha TPHPA  kilichopo bandarini hapo zinazofanyika kwa ufanisi wa hali juu.  Akiongelea kuhusu uboreshwaji uliofanywa na  Serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha Miundo mbinu kwa kuongeza kina cha bahari ambapo sasa Meli kubwa zinaingia katika Bandari  hivyo kwa wale wananitumia Bandari ya Mombasa wasisite kupitisha hapa mazao yao, aidha  wataepuke changamoto mbalimbali za kiutaratibu ikiwepo kuhakikisha mazao yamekaguliwa katika kituo cha TPHPA na kupata nyaraka za uthibitisho.  Akiongelea kuhusu changamoto mbalimbali zitokanazo na wateja wao amesema changamoto kubwa ni uelewa wa utaratibu za kufuata ili kusafirisha mazao lakini kwa  wamek...

Naibu Waziri Mhe. Silinde aiagiza TPHPA kuweka Kontena lenye Ofisi na Maabara ya Kisasa Mpaka wa Sirari

Image
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb), alikitembelea Kituo cha Ukaguzi cha Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kilichopo Mpaka wa Sirari, wilayani Tarime, mkoani Mara, tarehe 24 Januari 2025, na kutoa maelekezo muhimu ya kuboresha utendaji wa kituo hicho. Katika ziara yake, Mhe. Silinde alielekeza TPHPA kuleta kontena litakalofanyiwa ofisi na maabara ya kisasa, yenye vifaa vyote muhimu kwa ajili ya ukaguzi wa mazao. Kontena hilo litakuwa na teknolojia ya kisasa itakayosaidia kuongeza ufanisi katika shughuli za ukaguzi, akiongeza kuwa kontena hilo litapelekwa kwenye kituo hicho mwezi Februari 2025. Pia, Mhe. Silinde aliwahimiza wafanyakazi wa kituo hicho kufanya kazi kwa ufanisi, umakini na usawa ili kuboresha huduma zinazotolewa. "Kazi zenu ni muhimu kwa uchumi wa taifa na ni lazima zitekelezwe kwa kiwango cha juu cha ufanisi," alisisitiza. Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Prof. Joseph Nduguru, alikiri kupokea maelekezo hayo na kueleza kuwa kontena hilo...

NAIBU WAZIRI SILINDE AIAGIZA TPHPA KUJENGA MAABARA ZA KISASA KATIKA VITUO VYA UKAGUZI RUSUMO NA MUTUKULA

Image
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb), ameielezeka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kujenga Maabara za Kisasa katika vituo vya ukaguzi vilivyopo katika mipaka ya Rusumo (Ngara) na Mutukula, ili kuboresha utendaji kazi wa vituo hivyo na kuharakisha mchakato wa ukaguzi wa mazao. Mhe. Silinde alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika vituo hivyo vilivyopo mkoani Kagera tarehe 23 Januari 2025. Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kukagua utendaji kazi wa vituo hivyo, kubaini changamoto zinazojitokeza na kuzitolea ufumbuzi ili kuongeza ufanisi wa shughuli zinazofanyika katika mipaka hiyo ya biashara. Akizungumza na viongozi wa TPHPA, Naibu Waziri Silinde alieleza kuwa, ujenzi wa maabara za kisasa katika vituo vya Rusumo na Mutukula utahakikisha kuwa huduma za ukaguzi na utoaji wa vyeti vya usafi wa mazao zinafanyika kwa haraka na kwa ubora wa hali ya juu, huku akisisitiza umuhimu wa maabara hizo katika kuhakikisha usalama wa mazao yanayo...