WASAFIRISHAJI WA MAZAO WAHIMIZWA KUTUMIA BANDARI YA TANGA,WAHAKIKISHIWA KUWEPO HUDUMA BORA ZA UKAGUZI KUTOKA TPHPA
Hayo yamesemwa na Kaimu Afisa Mfawidhi wa Kituo cha TPHPA kilichopo Bandari ya Tanga Bi Monica Sylvester Kuziwa ambapo amewataka Wasafirishaji wa mazao nchini kuwa wazalendo na kutumia Bandari ya Tanga kusafirisha mazao yao na kupata huduma bora za ukaguzi wa mazao hayo inayotelewa na Ofisi ya Kituo cha TPHPA kilichopo bandarini hapo zinazofanyika kwa ufanisi wa hali juu.
Akiongelea kuhusu uboreshwaji uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha Miundo mbinu kwa kuongeza kina cha bahari ambapo sasa Meli kubwa zinaingia katika Bandari hivyo kwa wale wananitumia Bandari ya Mombasa wasisite kupitisha hapa mazao yao, aidha wataepuke changamoto mbalimbali za kiutaratibu ikiwepo kuhakikisha mazao yamekaguliwa katika kituo cha TPHPA na kupata nyaraka za uthibitisho.
Akiongelea kuhusu changamoto mbalimbali zitokanazo na wateja wao amesema changamoto kubwa ni uelewa wa utaratibu za kufuata ili kusafirisha mazao lakini kwa wamekuwa wakitoa elimu kwa wasafirishaji ili kuwaelimisha jambo ambalo limekuwa likisaidia katika kupunguza changamoto hizo.
Comments
Post a Comment