TPHPA Yaandaa Kizazi Kipya cha Wataalamu wa Kilimo Salama Kupitia Mafunzo kwa Vitendo

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) inaendelea kuwa daraja muhimu la maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini kupitia programu yake ya mafunzo kwa vitendo. Kupitia programu hii, wanafunzi hupata nafasi ya kujifunza kwa vitendo masuala ya udhibiti wa visumbufu vya mimea, usimamizi wa viuatilifu, afya ya mimea, karantini na taratibu za usafirishaji wa mazao, hivyo kuongeza uelewa wao wa nadharia na vitendo. Katika vituo vya TPHPA vilivyopo Makao Makuu Ngaramtoni, maabara ya Kibaha, pamoja na ofisi za kanda, wanafunzi hushirikiana bega kwa bega na wataalamu wa mamlaka hiyo katika shughuli za tafiti, ukaguzi wa viuatilifu, na utoaji wa elimu kwa wakulima. Pia hujifunza mbinu za uchambuzi wa viuatilifu na matumizi ya teknolojia za kisasa katika maabara, ikiwemo uchunguzi wa mabaki ya viuatilifu kwenye mazao na mazingira, jambo linalowawezesha kupata ujuzi wa kiufundi na wa kitaalamu. Kupitia mpango huu, TPHPA inalenga kuandaa kizazi kipya cha...