Mashirika ya Umma yasiyoshiriki Mashindano ya SHIMMUTA kikaangoni,Naibu Waziri Mkuu Mhe. Biteko atoa Maagizo

Na Innocent Natai Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amemtaka Msajili wa Hazina kufikia Jumanne asubuhi awasilishe maelezo ya kwa nini mashirika mengi ya Umma hayajashiriki Michezo ya SHIMMUTA inayoendelea jijini Dodoma, huku ikitambulika kuwa, mashindano hayo yalianzishwa na Serikali huku mlezi wake akiwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma wakati akifungua Mashindano ya SHIMMUTA yanayohusisha Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi ambapo awali, Mwenyekiti wa Kamati ya SHIMMUTA, Roselyne Massama alimweleza Naibu Waziri Mkuu kuwa wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya muitikio mdogo wa Mashirika ya Umma kushiriki mashindano hayo jambo ambalo linazorotesha mashindano hayo. “‘Viongozi Serikali kama tumekubaliana kufanya jambo fulani basi tulifanye, na kama tunaona halifai basi bora tuliache, kuliko tunakubaliana kufanya kitu halafu hatukifanyi, haiwezekani viongozi w...