WATUMISHI TPHPA WA JENGEWA UWEZO WA MATUMIZI YA MFUMO WA OFISI MTANDAO (E- OFFICE)
Na Innocent Natai
Leo Novemba 7. 2023 Wafanyakazi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania(TPHPA) wamejengewa uwezo juu ya matumizi ya mfumo wa TEHAMA (Mfumo wa Ofisi Mtandao E- Office),mafunzo hayo yameendeshwa katika Ofisi za Mamlaka zilizopo Arusha Ngaramtoni
Wafanyakazi hao wameshukuru kwa mafunzo hayo ambapo wameipongeza serikali kwa kuanzisha mfumo huu unaoenda kuipunguzia Mamlaka gharama za uendeshaji kuanzia kudurufu makabrasha
Dkt. Sospeter Kabululu ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA amesema kuwa, mfumo huu utakuwa na manufaa kwa sababu unaenda kupunguza gharama za kuandaa makrabasha, itaokoa muda, huku akiwataka Wafanyakazi hao kuutumia mfumo huu kwa kadri ya maelekezo yatakayotolewa.
Akitaja faida za mfumo huo amesema kuwa Mfumo wa Ofisi Mtandao umetengenezwa ili kuwezesha na kurahisisha shughuli za utawala za kila siku ndani ya Serikali. Shughuli hizo zinahusu mzunguko wa mafaili na nyaraka ndani na miongoni mwa taasisi za umma.
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kupitia kitengo cha TEHAMA imeendelea kuboresha matumizi ya TEHAMA ambapo imefanikiwa kuanza na kutumia mifumo mbalimbali itakayoiwezesha mamlaka kutoa huduma kwa urahisi kwa wananchi
Mfumo huu wa Ofisi Mtandao ‘e-office’ umesainifiwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwa kushirikiana na Idara ya Nyaraka na Kumbukumbu za Taifa (RAMD) ambao wanasimamia taratibu na mifumo ya Masjala nchini.
Comments
Post a Comment