MAFUNZO YA 59 YA PM2 YALIYOTOLEWA NA TPHPA JIJINI ARUSHA YAFUNGWA RASMI LEO,UPIMAJI WA UELEWA KWA WASHIRIKI WATOA MATOKEO MAZURI






Na Mariam Makombe

Hayo yamejiri leo 17 novemba katika ukumbi wa Mamlaka uliopo Makao Makuu Ngaramtoni Arusha ambapo Kaimu Mkurugenzi Dr.Osmundi Ndomba ameyafunga mafunzo hafla iliyoshuhudiwa pia  na wajumbe wa Menejimenti.

Akiongea katika hafla hiyo Mratibu wa mafunzo ndg.Jumanne amesema mafunzo hayo yamekuwa na matokeo mazuri sana ambapo upimaji wa awali siku ya Kwanza na wa mwishoni umetofautiana na matokeo  ya mwisho yamekuwa mazuri ambapo washiriki wamejibu maswali Kwa ufasaha ikionyesha ni ushahidi walielewa wanachofundishwa, akileta maombi yake kama mratibu kwa Mamlaka katika hotuba yake amesema anaomba ufanyike utaratibu wa kuundwa umoja wa wauza pembejea kila mkoa kwani italeta mafanikio makubwa katika kudhibiti .Pia ameomba kuongezea Kwa idadi ya Wakaguzi katika maduka ya Viuatilifu ili kuleta tija zaidi.

Aidha Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Viuatilifu Dr  Oshingi Shilla akiongea katika hafla hiyo amewataka washiriki hao kwenda kutangaza Mamlaka ,pamoja na hilo amewataka iwapo wataenda kukumbana na uvunjifu wa sheria kwa wafanyabiashara wengine wasisite kutoa taarifa lakini pia wahakikishe wanatumia mfumo wa ATMIS ili kuisaidia Mamlaka kuboresha huduma zake,ameahidi pia kufanyia kazi changamoto zote ambazo watakuwa wameziwakilisha Kwa Mratibu .

Nae Mgeni rasmi Dr.Osmundi Ndomba akiongea wakati akifunga mafunzo hayo ametoa pongezi kwa timu nzima iliyoshiriki katika kila eneo kufanikisha mafunzo hayo,pili amesema pamoja na majukumu mengine kama kuwezesha biashara ya mazao kwa kuthibitisha ubora wa mazao yanayotakiwa Kusafirisha nje ya nchi ,kufanya utafiti wa Visumbufu na kutafuta mbinu za  udhibiti Mamlaka  pia ina jukumu la kuelimisha wakulima na Wafanyabiashara wa Viuatilifu juu ya matumizi sahihi ya Viuatilifu hivyo..

Aidha amewashukuru washiriki kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka kwa kushiriki mafunzo haya ya matumizi sahihi ya Viuatilifu  kwani ni moja  ya jukumu la Mamlaka  lakini amewataka waende kutoa mafunzo kwa wengine wasikae nayo  elimu waliyoipata bila kufundisha wengine,aidha amesema mafunzo haya yapo kisheria hivyo wazingatie miongozo waliyopewa. Sambamba na hilo amewataka kuwa makini katika utumiaji kwani Viuatilifu ni sumu vikitumika vibaya vinaweza kuleta madhara Kwa binadamu.

Akizungumzia suala la maombi ya kuongeza Wakaguzi Dr.Osmundi Ndomba amesema  Wakaguzi wanatakiwa kuweka msawazo kwa kufika maeneo ya vijijini hii ni moja ya njia ya kutatua upungufu huo wakati namna nyingine ikiangaliwa ya kutatua tatizo hilo ,lakini pia amesisitiza mafunzo haya kufanyika maeneo ya vijijini ili wote waweze kuelimika na mafunzo haya na hatimae kufikia lengo.

Mshindi wa Kwanza hadi watatu  katika upimaji wamekabidhiwa zawadi za vifaa kinga kama moja ya motisha kutokana na ufahulu mzuri kwenye upimaji,nao washiriki katika risala yao wameishukuru  Mamlaka Kwa mafunzo hayo na kutaka yaendelee sehemu zingine ili kuweza kuleta tija katika kilimo,pamoja na zawadi hizo washiriki wote wamepewa vyeti vya kufuzu mafunzo hayo ya matumizi sahihi ya Viuatilifu.

Mafunzo haya ni ya 59 tangu yalipoanza mwaka 1994,na  yataendelea kutolewa maeneo mbalimbali ili kuleta tija katika afya ya mimea,ili kupata matangazo ya mafunzo haya tembelea mitandao yetu ya kijamii tphpa_tz Instagram ,YouTube TPHPA HABARI TV

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu