Posts

Showing posts from June, 2024

MAFUNZO YA KUWA JENGEA UWEZO WA KUFANYA TATHMINI ZA VIUATILIFU; KAIMU MKURUGENZI MKUU TPHPA NDUGU OSHINGI SHILLA AWATAKA WASIMAMIZI WA VIUATILIFU KUZINGATIA MAFUNZO WATAKAYOPATA ILI KULETA UFANISI KATIKA KAZI ZAO

Image
Hayo yamejiri wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya namna ya uhakiki wa vihatarishi katika viuatilifu yanayoendelea katika ukumbi wa Kibo Palace ambapo Mgeni rasmi  Kaimu Mkurugenzi Mkuu ndugu Oshingi Shilla amefungua mafunzo hayo. Akiongea mara baada ya kufungua Mafunzo hayo ya kujengewa uwezo  kwa watumishi wanaohusika na usimamizi wa viuatilifu amesema ndg.Oshingi amesema lengo la afunzo haya ni kuendeea kuwajengea uwezo watumishi wanaohusika na usimamiaji wa viuatilifu nchinj ili kuwaongezea ujuzi katika usimamiaji na si hivyo tu bali pia  kuwataka wafuate utaratibu unaotakiwa katika uhakiki wa ubora wa viuatilifu na kutoa tathmini sahihi juu ya athari za viuatilifu ili kujua ubora na kuwakinga watumiaji wa viuatilifu ambao ni wa kulima.. Akiongelea kuhusu uwezeshaji endelevu kwa wasimamizi hawo amesema Mamlaka imejipanga na siku zote imekuwa ikifanya hivyo kuhakikisha mafunzo haya ni endelevu kwani  kumekuwa na mabadiliko ya  teknoloiia hivyo mafunzo hayo ni end...

TPHPA KUFIKIA MALENGO YA KUBORESHA AFYA ZA WALAJI

Image
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania   TPHPA imefanikiwa kuweka mikakati ya msingi inayolenga kuzalishwa mazao yasiyo na masalia ya Viuatilifu ili kupanua wigo katika soko la dunia kwa mustakabali wa kulinda afya za Binadamu na Mazingira. Akizungumza katika Mkutano wa Mwaka wa Wadau wa   Afya ya Mimea na Viuatilifu Uliofanyika Juni 21. 2024 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Mamlaka hiyo Ngaramtoni, Jijini Arusha ambao hufanyika kila mwaka, Mkuu wa   Wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda akimwakilisha Waziri wa Kilimo Hussein Bashe aliyetarajiwa kuwa Mgeni Rasmi, ameipongeza Mamlaka hiyo kwa jitihada zake kubwa za kuleta mabadiliko na uzalishaji wenye tija   katika Sekta ya Kilimo. Aidha ameongeza kuwa, Sekta ya Kilimo ni mkombozi kwani inategemewa kuongeza ajira za vijana na wanawake, kutoa ajira za stara, kuimarisha mfumo wa chakula na kuongeza pato la taifa kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030. "Serikali kwa kutambua umuhimu wa sekta hii muhimu imeongeza bajet...

TPHPA yazidi Kung'ara Maonesho ya Saba Saba,Waziri wa Nchi wa Ugatuzi na Masuala ya Mkoa nchi ya Zimbabwe afika kujionea

Image
Na Innocent Natai - Dar Es Salaam Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imeendelea kuwa kivutio katika  maonesho ya 48 ya  Kimataifa  ya Biashara maarufu kama (Saba Saba)  yaliyoanza Juni 28,2024 na kuzinduliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa nchi  ya  Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi Julai 3. 2024  hukuyakiongozwa na  kauli mbiu isemayo "Tanzania mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji"   ikilenga kuonesha Dunia kubwa serikali ya awamu ya sita ipo tayari  na inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa Ndani na nje ya nchi kufanya biashara na kuwekeza katika  sekta mbalimbali za uzalishaji ikiwemo sekta ya Viwanda,kilimo,teknolojia,uwekezaji na Utalii. Kutokana na huduma mbalimbali  Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA)  inazozitoa na elimu hususani fursa za biashara za mazao,  Mhe. Ruvai Ezi...