MAFUNZO YA KUWA JENGEA UWEZO WA KUFANYA TATHMINI ZA VIUATILIFU; KAIMU MKURUGENZI MKUU TPHPA NDUGU OSHINGI SHILLA AWATAKA WASIMAMIZI WA VIUATILIFU KUZINGATIA MAFUNZO WATAKAYOPATA ILI KULETA UFANISI KATIKA KAZI ZAO












Hayo yamejiri wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya namna ya uhakiki wa vihatarishi katika viuatilifu yanayoendelea katika ukumbi wa Kibo Palace ambapo Mgeni rasmi  Kaimu Mkurugenzi Mkuu ndugu Oshingi Shilla amefungua mafunzo hayo.

Akiongea mara baada ya kufungua Mafunzo hayo ya kujengewa uwezo  kwa watumishi wanaohusika na usimamizi wa viuatilifu amesema ndg.Oshingi amesema lengo la afunzo haya ni kuendeea kuwajengea uwezo watumishi wanaohusika na usimamiaji wa viuatilifu nchinj ili kuwaongezea ujuzi katika usimamiaji na si hivyo tu bali pia  kuwataka wafuate utaratibu unaotakiwa katika uhakiki wa ubora wa viuatilifu na kutoa tathmini sahihi juu ya athari za viuatilifu ili kujua ubora na kuwakinga watumiaji wa viuatilifu ambao ni wa kulima..

Akiongelea kuhusu uwezeshaji endelevu kwa wasimamizi hawo amesema Mamlaka imejipanga na siku zote imekuwa ikifanya hivyo kuhakikisha mafunzo haya ni endelevu kwani  kumekuwa na mabadiliko ya  teknoloiia hivyo mafunzo hayo ni endelevu ili kuendana na mabadiliko yanayotokea kutokana na kuingia kwa teknolojia .

Aidha amewashukuru Swedish Chemical Agency (KEMl )ambao pia ni  Washirika wao ambao wanasaidia katika kuwezesha mafunzo haya ndani ya nchi na nje ya nchi ambapo huwezesha pia baadhi ya watumishi kwenda kujifunza zaidi nchini Sweden.

Mafunzo haya ni endelevu na pamoja na mafunzo haya kutakuwa na miradi ya pamoja kati ya TPHPA na KEMI ambayo imepata ufadhiri kutoka Swedish development Agency (Sida) ili kuendelea kuimarisha usimamizi wa Viuatilifu nchini kuwa wenye tija na kufikia malengo ya Muda mrefu ya Mamlaka ya TPHPA.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu