Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Apokea Makombe 6 yaliyopatikana Katika Mashindano ya Mei Mosi na SHIMMUTA 2024











Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Profesa Joseph Ndunguru, amepokea jumla ya makombe 6 kutoka kwa Kamati ya Michezo ya Mamlaka hiyo, baada ya kufanya vyema katika mashindano mbalimbali yaliyofanyika kwenye mashindano ya SHIMMUTA jijini Tanga mwezi Novemba na sherehe za wafanyakazi (Meimosi 2024).

Katika mashindano hayo, Mamlaka ya TPHPA ilifanikiwa kutwaa makombe katika michezo tofauti, ikiwa ni pamoja na:

- Mchezo wa Bao: Mshindi wa Kwanza

- Darts: Mshindi wa Pili

- Karata: Mshindi wa Kwanza

- Kukimbia kwenye Gunia: Mshindi wa Kwanza

- Riadha: Mshindi wa Pili

Akizungumza na Watumishi wa Mamlaka, Profesa Ndunguru alitoa pongezi kwa wachezaji wote walioshiriki na kushinda, akisisitiza umuhimu wa michezo katika kuboresha mahusiano kazini, afya njema, na kuongeza ufanisi wa kazi. Aliwataka watumishi wengine kujiunga na michezo ili waweze kufurahia faida zake, kama vile kujenga umoja na kukuza ustawi wa mwili na akili.

Huu ni ushindi mkubwa kwa Mamlaka ya TPHPA, ukionyesha sio tu umahiri wa wachezaji wake bali pia dhamira ya taasisi hiyo katika kuboresha ustawi wa wafanyakazi wake kupitia michezo.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu