Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu














Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imevunja rekodi kubwa katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma, Taasisi, na Makampuni Binafsi (SHIMMUTA) 2024, yaliyofanyika mkoani Tanga. Mashindano haya ya 51 tangu kuanzishwa, yamejulikana kwa ushindani mkali, kujenga Afya za Watumishi na Ushirikiano miongoni mwao ukijumuisha ushiriki wa mashirika 95 na wanamichezo 4720 kutoka mashirika na Taasisi 


Leo Novemba 24,2024 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo, alifunga mashindano hayo na kusisitiza umuhimu wa michezo katika kukuza afya na ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi. 


TPHPA inajivunia mafanikio na inashukuru wachezaji wake kwa kuleta heshima na mafanikio makubwa katika mashindano haya ambapo Bi. Rhoda Simon wa TPHPA alionyesha umahiri mkubwa katika mbio za magunia, akishinda kwa kasi ya kipekee na kumaliza mbio hizo kwa muda wa sekunde 28, na hivyo kutwaa taji la ubingwa ambapo leo amekabidhiwa kombe. Aidha, Bi. Veneranda Edward amefanikiwakuingia kwenye historia kwa kutwaa ubingwa wa Bao kwa Wanawake, akimshinda mchezaji kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa pointi nyingi.


Hata hivyo TPHPA imefanikiwa kutwaa taji jingine kubwa kwa kuwa mshindi wa pili katika mchezo wa Vishale(Darts), ambapo Bi. Rehema Abdala, aliyefanikiwa kuingia fainali kuwa Mshindi wa pili baada yakushindwa kushiriki katika fainali hiyo kutokana na matatizo ya kifamilia.


TPHPA imeweka rekodi ya kipekee baada ya kuzidi Taasisi na Mashirika yenye Makao Makuu katika Mikoa ya Kaskazini kwa idadi kubwa ya Makombe,Imetoa Mshindi wa Mbio za Magunia Wanawake aliyekimbia kwa Muda Mfupi tangu kuanzishwa kwa Mashindano,Mshiriki wa mchezo wa Vishale Wanawake aliyeshinda Michezo yake yote hadi Fainali


Kwa ujumla, mashindano haya yameonyesha umuhimu wa michezo katika kuleta pamoja wafanyakazi kutoka sekta mbalimbali na kuimarisha afya na ushirikiano katika jamii ya wafanyakazi nchini. TPHPA inatoa wito kwa mashirika mengine kuendelea kuhimiza michezo na shughuli za kijamii kama njia mojawapo ya kuimarisha ustawi wa wafanyakazi na jamii kwa ujumla.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO