TPHPA YATUMIA KONGAMANO LA PEMBEJEO MKOANI MBEYA KUWAASA WAKULIMA JUU YA MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA VIUATILIFU

Akifungua Kongamano hilo litakalofanyika kwa siku mbili Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi amewapongeza taasisi ya CropLife Tanzania kwa kuandaa kongamano hilo mkoani hapo kwani litawasaidia wakulima wengi kwa kuwaongezea uwezo na kuzidi kuimarisha uzalishaji wa mazao bora ya biashara pamoja na chakula. Ikiwa kama mshiriki mkuu wa Kongamano hilo, Mamlaka ya Afya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imetumia uwanja wa Kongamano hilo kuwafundisha wakulima matumizi Sahihi na Salama ya Viautilifu, Utambuzi wa visumbufu mbalimbali pamoja na njia za kuwadhibiti. Mdhibiti Ubora wa Viuatilifu kutoka TPHPA Ndg.Ramadhani Kilewa amewaasa wakulima kuzingatia maelezo yanayoandikwa kwenye vibandiko vya viuatilifu ili kuepusha matumizi ya Viuatilifu bandia, Kukosea na kutumia kiuatilifu kisichoendana na zao au visumbufu husika na pia Kujikinga dhidi ya Madhara yatokanayo na kutotumia viuatilifu kwa Usahihi na Usalama kwani viuatilifu hivi ni Sumu. Uwepo wa TPHPA Kongamano hilo unasisit...