Taasisi mbalimbali za Kimataifa zazidi kumiminika TPHPA kufanya Mashirikiano
Lengo kuu la ziara hii ni kujifunza kutoka kwa uzoefu wa TPHPA katika kudhibiti na kudumisha viwango vya ubora wa mazao, hususan katika masuala ya usalama wa chakula na biashara za mazao ya kilimo. Wakati wa ziara, pande zote mbili zilijadili mikakati bora ya udhibiti wa magonjwa ya mimea na usalama wa chakula, na kubadilishana mawazo kuhusu mbinu bora za kuongeza ufanisi katika sekta ya kilimo.
Prof. Ndunguru alielezea furaha yake kupongeza hatua hii ya ushirikiano, akisema kuwa ni muhimu kwa nchi zote kushirikiana ili kuboresha udhibiti wa afya ya mimea na kuhakikisha mazao yanayoingia na kutoka nchi hizo yanakuwa salama kwa matumizi ya binadamu. TPHPA itaendelea kutoa msaada na ushauri wa kitaalam ili kuongeza nguvu katika juhudi za kimataifa za kulinda usalama wa chakula.
Comments
Post a Comment