Posts

Showing posts from June, 2025

Dkt. Oshingi Shilla Afunga Mafunzo ya Wakaguzi wa Afya ya Mimea na Viuatilifu, Awasisitiza Weledi, Uadilifu na Utoaji wa Haki

Image
Leo Juni 18, 2025, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Dkt. Oshingi Shilla, amefunga rasmi mafunzo ya wakaguzi wa afya ya mimea na viuatilifu yaliyofanyika kwa muda wa siku 10 katika ukumbi wa Maji House, Morogoro. Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Dkt. Shilla amewasisitiza washiriki kuwa na weledi, uadilifu na kuhakikisha utoaji wa haki wakati wa kuwahudumia wananchi. Katika mafunzo hayo, washiriki walipatiwa elimu kuhusu mifumo ya kisheria, taratibu za ukaguzi, mnyororo wa ushahidi (chain of custody), mifumo ya kikodi kutoka TRA, pamoja na matumizi ya mfumo mpya wa e-Kilimo. Mratibu wa mafunzo hayo, Ndugu Mussa Chidinda, alieleza hayo mbele ya mgeni rasmi, akisisitiza kuwa lengo kuu ni kuwawezesha wakaguzi hao kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi. Mafunzo haya yamehusisha wakufunzi kutoka ndani na nje ya Mamlaka na yamewahusisha jumla ya washiriki 70 ambao ni watumishi wa TPHPA kutoka kanda zote saba za Mamlaka. Aidha, vion...

Watumishi wa TPHPA waendelea kunolewa katika mafunzo ya ukaguzi wa Afya ya Mimea na Viuatilifu

Image
Leo Juni 14, 2025, watumishi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) wanaoendelea na mafunzo ya ukaguzi wa afya ya mimea na viuatilifu wamepatiwa mafunzo kuhusu Legal Procedures and Chain of Custody, yaliyotolewa na Afisa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Mafunzo hayo yamewapa uelewa kuhusu taratibu za kisheria katika ushughulikiaji wa ushahidi na usalama wa mnyororo wa ushahidi kuanzia eneo la tukio hadi kufikishwa kwa mamlaka husika. Aidha, washiriki wameelimishwa pia kuhusu mifumo mbalimbali ya kikodi na taratibu za kodi kutoka kwa Afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa lengo la kuongeza uelewa juu ya wajibu wa kikodi kwa taasisi na wafanyabiashara wa viuatilifu. Mafunzo haya yanahakikisha wakaguzi wanakuwa na ujuzi wa kina na uelewa mpana unaowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi mkubwa.