Dkt. Oshingi Shilla Afunga Mafunzo ya Wakaguzi wa Afya ya Mimea na Viuatilifu, Awasisitiza Weledi, Uadilifu na Utoaji wa Haki
Katika mafunzo hayo, washiriki walipatiwa elimu kuhusu mifumo ya kisheria, taratibu za ukaguzi, mnyororo wa ushahidi (chain of custody), mifumo ya kikodi kutoka TRA, pamoja na matumizi ya mfumo mpya wa e-Kilimo. Mratibu wa mafunzo hayo, Ndugu Mussa Chidinda, alieleza hayo mbele ya mgeni rasmi, akisisitiza kuwa lengo kuu ni kuwawezesha wakaguzi hao kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Mafunzo haya yamehusisha wakufunzi kutoka ndani na nje ya Mamlaka na yamewahusisha jumla ya washiriki 70 ambao ni watumishi wa TPHPA kutoka kanda zote saba za Mamlaka. Aidha, viongozi wa idara, vitengo na kanda mbalimbali pia walichangia kuwajengea uwezo washiriki kwa kutoa mada na miongozo mbalimbali ya kiutendaji.
Kwa pamoja, TPHPA inaamini kuwa mafunzo haya yatakuwa kichocheo cha utekelezaji bora wa majukumu ya wakaguzi katika kulinda afya ya mimea, usalama wa chakula na mazingira nchini.
Comments
Post a Comment