Watumishi wa TPHPA waendelea kunolewa katika mafunzo ya ukaguzi wa Afya ya Mimea na Viuatilifu








Leo Juni 14, 2025, watumishi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) wanaoendelea na mafunzo ya ukaguzi wa afya ya mimea na viuatilifu wamepatiwa mafunzo kuhusu Legal Procedures and Chain of Custody, yaliyotolewa na Afisa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Mafunzo hayo yamewapa uelewa kuhusu taratibu za kisheria katika ushughulikiaji wa ushahidi na usalama wa mnyororo wa ushahidi kuanzia eneo la tukio hadi kufikishwa kwa mamlaka husika.

Aidha, washiriki wameelimishwa pia kuhusu mifumo mbalimbali ya kikodi na taratibu za kodi kutoka kwa Afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa lengo la kuongeza uelewa juu ya wajibu wa kikodi kwa taasisi na wafanyabiashara wa viuatilifu.

Mafunzo haya yanahakikisha wakaguzi wanakuwa na ujuzi wa kina na uelewa mpana unaowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi mkubwa.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu