"TUTAMPIGA YEYOTE ATAKAYEKUJA MBELE YETU" Timu ya mpira wa miguu ya Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania yaendelea na Mazoezi



Picha Mbalimbali zikionyesha Wafanyakazi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA FOOTBALL CLUB) wakipokea maelekezo kutoka kwa Kocha Mkuu na kufanya mazoezi katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Mringa  Wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha












Na Innocent Natai :Arusha

Timu ya mpira wa miguu ya Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA FOOTBALL CLUB) leo Tarehe 8 Novemba,2022 katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Mringa  Wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha imeendelea kujiada kwa ajili ya kushiriki mashindano ya SHIMMUTA 2022 yatakayofanyika Mkoani Tanga mwanzoni mwa mwezi huu

Akizungumza na TPHPA Habari Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Mamlaka Ndg.Remijus Mchunguzi amesema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na wachezaji wameonekana kuanza kuzinasa mbinu za Kocha na Kuzifanyia kazi

"Wachezaji wote wameonekana kuwa wenye  morali ya kusaka pointi 3 katika kila mchezo unaowajia mbeleni katika michuano hii muhimu, ambazo zitaiweka  timu katika mazingira mazuri ya kutwaa Ubingwa"Ndg.Remijus

Aidha ameongeza kuwa Kocha Mkuu  amefurahishwa na nidhamu ya hali ya juu kwa wachezaji wake, kwani wachezaji wote wameweza kufanya mazoezi ya leo kwa bidii, na wachezaji wachache ndio wameshindwa kushiriki mazoezi kutokana na majeraha madogo madogo ambayo hayatawaweka nje kwa muda mrefu bali watarejea mazoezini




Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu