HABARI PICHA :WATUMISHI WA MAMLAKA WAENDELEA KUPATIWA ELIMU YA MATUMIZI YA MFUMO WA ULIPAJI SERIKALINI (MUSE)
Na Innocent Natai
JANUARI 19/2023 Picha na Matukio mbalimbali zikionyesha washiriki wa mafunzo ya Mfumo wa Ulipaji Serikalini(MUSE) yanayoendelea katika Ofisi za Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania zilizopo Arusha ,Kukamilika na kuanzwa kutumiwa kwa Mfumo huo kunatarajiwa kusaidia kuongeza makusanyo ya mapato, utarahisisha ulipaji wa fedha pamoja na kutunza kumbukumbu za matumizi ya fedha.
Aidha Mafunzo hayo yamewahusisha Wahasibu, Meneja wa Fedha, Wataalam wa Manunuzi, Maafisa TEHAMA na Maafisa Bajeti,Mafunzo hayo ya natarajiwa kumalizika ndani ya wiki mbili yakilenga kuwajengea uwezo wa kuutumia vilivyo mfumo huo.

Comments
Post a Comment