Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imevunja rekodi kubwa katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma, Taasisi, na Makampuni Binafsi (SHIMMUTA) 2024, yaliyofanyika mkoani Tanga. Mashindano haya ya 51 tangu kuanzishwa, yamejulikana kwa ushindani mkali, kujenga Afya za Watumishi na Ushirikiano miongoni mwao ukijumuisha ushiriki wa mashirika 95 na wanamichezo 4720 kutoka mashirika na Taasisi Leo Novemba 24,2024 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo, alifunga mashindano hayo na kusisitiza umuhimu wa michezo katika kukuza afya na ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi. TPHPA inajivunia mafanikio na inashukuru wachezaji wake kwa kuleta heshima na mafanikio makubwa katika mashindano haya ambapo Bi. Rhoda Simon wa TPHPA alionyesha umahiri mkubwa katika mbio za magunia, akishinda kwa kasi ya kipekee na kumaliza mbio hizo kwa muda wa sekunde 28, na hivyo kutwaa taji la ubingwa ambapo leo amekabidh...
Comments
Post a Comment