"TPHPA tumejipanga kuhakikisha tunatimiza adhma ya Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ya Tanzania tuilishe dunia" Prof Joseph Ndunguru

Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano TPHPA
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania(TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru amesema kuwa Mamlka hiyo imejipanga kuhakikisha inaboresha mazingira ya utoaji wa huduma za afya ya mimea mipakani na kutimiza adhima ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ya Tanzania tuilishe dunia katika mazao yale ambayo ni ya chakula ili kurahisisha biashara za mazao ya kilimo
Prof. Joseph Ndunguru ameyasema hayo Katika siku ya pili ya ziara yake ya kutembelea vituo vya Mamlaka,ambapo leo Mei 4/2023 amefanya ziara katika kituo cha ukaguzi cha TPHPA(Tarake) kilichopo baina ya Tarakea Wilayani Rombo, Mkoani Kilimanjaro na Nchi ya Kenya,Ziara hiyo pamoja na mambo mengine ililenga kukagua na kutatua changamoto za vituo vya Mamlaka hiyo,katika ziara hiyo aliambatana na Mkurugenzi wa huduma saidizi TPHPA Ndug.Ahmada Suleman
“Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, imedhamiria kuhakikisha inaongeza mauzo ya nje ya chakula mwaka hadi mwaka na kama Mamlaka tunataka kutimiza adhima ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ya Tanzania tuilishe dunia katika mazao yale ambayo ni ya chakula na itawezekana kwa sisi Mamlka kuboresha huduma za afya ya mimea na Watumishi kujituma ” alisema Prof. Joseph Ndunguru akizungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo Mpaka wa Tarakea
Comments
Post a Comment