"Tutaimarisha Masoko ya Mazao yetu kwa kupunguza Viuatilifu vyenye Madhara Makubwa kwa Binadamu na Mzingira" Prof.Kweka


Pichani: Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Prof. Eliningaya Kweka(Aliyesimama) akifungua Kikao cha Wataalamu kutoka TPHPA, Wizara ya Afya, Hospitali za Rufaa, Mkemia Mkuu wa Serikali, Mazingira na wadau wengine wa Kilimo na Viuatilifu Leo Juni 22,2023, Hoteli ya Gold Crest -Arusha.










Na Innocent Natai - TPHPA

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA)kwa kushirikiana na Wataalamu wa Afya na Mazingira  wamekutana Leo Juni 22,2023 katika Hoteli ya Gold Crest -Arusha kuandaa mikakati ya kupitia Viuatilifu vyenye madhara makubwa na ya muda mrefu kwa Mazingira na Binadamu vinavyopelekea Matukio ya Watu kutumia Kujiuwa 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Prof. Eliningaya Kweka amesema kuwa malengo makubwa ni kuona namna ya kuviondoa viuatilifu hivyo vyenye madhara ya muda mrefu kwa mazingira na Binadamu 

Hii ni ili kuhakikisha Wakulima wanakuwa Salama na Mazao yanayolimwa Tanzania yanalimwa kwa kutumia viuatilifu visivyo na madhara makubwa na yamuda Mrefu ili nchi kujihakikishia masoko ya Kimataifa kwa kuuza mazao yasio na Masalia ya viuatilifu vyenye madhara makubwa na ya muda mrefu kwa Binadamu na Mazingira

Mratibu wa Mradi wa Kupitia Viuatilifu vyenye Madhara Makubwa kwa Binadamu na Mazingira ambao umezinduliwa hivi leo katika kikao hicho kilichofanyika Arusha Ndug.Raphael Mwezi amesema kuwa wadau waliojumuika kwenye kikao hicho ni kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali,Wizara ya Afya,Hospitali za Rufaa MountMeru na KMCMC lengo ikiwa ni kutekeleza kwa pamoja mradi wa kudhibiti Viuatilifu vyenye athari kubwa kwa Binadamu na Mazingira ambavyo vimeripotiwa kwenye matukio ya Watu kujiuwa 

Aidha amesema kuwa lengo mahususi la mkutano huo wa kwanza wa Mradio huo ni kutengeneza mpango kazi wa namna gani wamaweza kuvitambua Viuatilifu hivyo na kuvifanyai utaratibu wa kuvipunguza 

Akizungumzia sakata la baadhi ya watu kutumia viuatilifu kujidhuru(kujiuwa) Daktari wa Afya ya Jamii kutoka Hospitali ya Rufaa ya KCMC Dkt.Florida Muro amesema kuwa kwa sasa takwimu sahihi za vifo na madhara yatokanayo na Viuatilifu hakuna hivyo mradi huo utasaidia kupatikana kwa takwimu sahihi na kujaribu kuviondoa viuatilifu hivyo

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu