WAFANYAJI SHUGHULI ZINAZOTUMIA VIUATILIFU WATAKIWA KUFANYA UPIMAJI KUGUNDUA MASALIA YA VIUATILIFU KATIKA MIILI YAO UPIMAJI
Mtaalam wa Maabara kutoka TPHPA Ndg.Raphael Mwezi amewataka wafanyaji shughuli zinazoambatana na matumizi ya Viuatilifu kufanya upimaji ili kubaini kama kuna masalia ya Viuatilifu katika miili yao ili kuwahi mapema matibabu kabla mwilibhaujadhurika zaidi hata kupelekea kifo.
Akielezea shughuli za sehemu ya kitengo hicho amesema kumekuwa na matumizi yasiyo sahihi ya utumiaji WA Viuatilifu ambapo imekuwa ikipelekea madhara makubwa kwa wahusika akielezea madhara hayo amesema sumu iliyopo kwenye Viuatilifu huingia katika mwili wa binadamu kupitia hewa,midomo,ngozi ambapo sumu ikiingia husambaa katika mfumo WA damu na kuweza kusababisha kifo,ulemavu wa kudumu,saratani ambayo huweza kuja kuonekana baada ya miaka 10-20 ,matatizo ya ini na hata michubuko kwenye mapafu.
Katika kuliona hili TPHPA(Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu )wamejikita katika kudhibiti hali hii Kwa njia mbalimbali,Kwanza ni kutoa elimu kwa watumiaji wa Viuatilifu hivi ambapo Mamlaka hukaribisha maombi kupitia barua Pepe dg@tphpa.go.tz au simu ya bure 0800110031 au kufika ofisini kutoka kwa mtu mmojammoja,vikundi au kampuni ili kupatiwa mafunzo ya namna bora ya utumiaji wa viuatilifu kwa gharama nafuu,
Pili ni kufanya upimaji kwa watumiaji ili kubaini kiwango cha masalia ya Viuatilifu katika miili yao na kuwashauri hatua za kuchukua mapema ili kuepuka madhara zaidi ambapo upimaji huu hugharimu kiasi cha shilingi 40000/=.
Hivyo watumiaji mnakaribishwa kwa ajili ya kupata huduma hii ili kuwa salama kwani afya zetu ni kipaumbele chetu tuzijali.
Comments
Post a Comment