Zoezi la Kudhibiti Kwelea Kwelea Mkoa wa Manyara, Wakulima watuma Ujumbe kwa Uongozi wa TPHPA na Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan











Na Innocent Natai


  SERIKALI kupitia Mamlaka ya Afya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imefanikiwa kudhibiti Makundi ya Ndege waharibifu aina ya Kwelea Kwelea zaidi ya Milioni 5 na kuokoa zaidi ya Ekari 1000 za zao la mpunga lililolimwa kipindi cha kiangazi Mkoani Manyara, na kuvamiwa na visumbufu hivyo mwanzoni mwa mwezi Septemba.

 

Akizungumza wakati wa kukamilisha opeshezani hiyo ya kudhibiti visumbufu hivyo Mtaalamu wa Kudhibiti visumbufu vya Mlipuko kutoka TPHPA Bwana Gladman Mbukoi amesema zoezi hilo limemaliza kilio cha wakulima wa mpunga kwani kwa siku moja ndege hao walikuwa na uwezo wa kumaliza zaidi ya Tani 50 za zao hilo.


Mbukoi amesema katika mkoa huo wamemaliza ndege hao kwa asilimia kubwa na kwamba operesheni hiyo haikuwa nyepesi kutokana na wingi wa ndege hao na kwa siku nne za oparesheni hiyo walikuwa wakifuatilia wanapolala ndege hao na kuwapulizia Vi-uatilifu ili kuwaangamizia wote lengo likiwa kuondolea wakulima usumbufu wa kutafuta walinzi wengi mashambani


Mariam Gadiel ambaye ni Mkulima mkoani hapo ameishukuru Mamlaka hiyo na Serikali kwa ujumla kwa kuwasaidia kudhibiti ndege hao kwani hapo awali walikuwa wakitumia gharama kubwa kufanya uzalishaji kwa kuwalipa walinzi sita kwa ekari moja, kwa kila mmoja walilazimika kumlipa shilingi laki moja kwa ajili ya kulinda ndege hao.


"Tunaishukuru Mamlaka ya Afya ya Mimea na Serikali ya Mama Samia hawa ndege walikuwa ni wasumbufu tulihamia mpaka na familia shambani kulinda mpunga sasa hivi tunapata hata muda wa kwenda nyumbani kuwapikia watoto wetu" aliongeza Mariam


Kaimu Meneja TPHPA Kanda ya Kaskazini Ndugu Jumma Mwinyimkuu, alisema kuwa visumbufu hivyo husababisha kupungua kwa tija kwa Mkulima katika uzalishaji, hivyo Mamlaka hiyo imejipanga kupambana na Visumbufu vya Mlipuko vitakavyo jitokeza ili kutekeleza lengo la Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha tija kwa wakulima inaongezeka ili kuilisha Dunia.


Ameongeza kuwa Mamlaka hiyo inavyotekeleza wajibu wake huo wakudhibiti visumbufu inaendana sambamba pia na niadhabiti ya Wizara ya kilimo katika kuhakikisha inaongeza Uzalishaji kwa wakulima na kuepuka kuwepo kwa tatizo la njaa nchini.


Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Usimamizi wa Visumbufu vya Mlipuko Ndugu, Godlove Kirimbo amesema kuwa Mamlaka hiyo imeweka mipango madhubuti kuhakikisha visumbufu hivyo havileti madhara makubwa kwa wakulima, kwa kushirikiana  wa wadau wa maendeleo kama Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wamenunua tayari Ndege Nyuki (Dron) zitakazo tumika kufanya ukaguzi wa kujua vilipo visumbufu na kuvipulizia viuatilifu aidha pia mamlaka hiyo inaendelea na mipango ya kununua ndege kwa ajili ya kufanya udhibiti huo wa visumbufu na inampango wakuandaa mfumo maalumu utakaotumiwa na wakulima kutoa taarifa za uwepo wa visumbufu ili kupata huduma kwa uharaka

 

 

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu