HAFLA YA MAKABIDHIANO VIFAA VYA UBORESHAJI AFYA YA MIMEA YAFANA, KAIMU MKURUGENZI ABAINISHA MANUFAA YATAKAYOPATIKANA,AMTAJA RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN
Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA)imepokea msaada wa vifaa wenye thamani ya Bil.2.2 kutoka FAO 10/10/2023 ambapo Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo Mh.David Silinde.
Akizungumza katika hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi wa TPHPA Prof.Joseph Ndunguru pamoja na kuishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kuwa mistari wa mbele kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo Kwa lengo la kuongeza ajira,kutanua masoko na hata kuiongezea Bajeti Wizara ya kilimo
Pia amebainisha mafanikio yatakayopatikana kutokana na vifaa hivyo ambapo amesema vifaa hivyo vitadaidia katika kuongeza maduhuli ya Serikali Kwa maana ya kuongeza mapato kutokana na ufanisi utakaoongezeka kutokana na vifaa hivyo kurahisisha utendaji wa kazi ambapo upande wa magari yatasaidia katika ufuatiliaji katika katika ukaguzi ,aidha vifaa vitasaidia katika kudhibiti na uhakika wa chakula na malighafi ya viwanda,mbali na Hilo vitasaidia kugundua visumbufu vipya na kuvidhibiti hivyo kupelekea Kupunguza upotevu wa mazao kabla na baada ya kuvunwa.
Mbali na hayo amesema itapelekea kufunguka kwa masoko mapya ya kilimo kwani udhibiti wa visumbufu itapelekea ubora wa mazao yatakayokuwa na ubora utakaofanya mazao yetu kukubalika na masoko ya nje hivyo kupelekea kufunguka kwa masoko ambapo ndio dhamira kubwa pia ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuona sekta ya Kilimo inakua na kuleta mafanikio Kwa wakulima wanapata masoko ya mazao yao nje ya nchi na kuboreka kwa maisha yao kwa ujumla
Comments
Post a Comment