KEMI Waahidi kuendeleza Mashirikiano na TPHPA //Wafanya ziara Kujionea Shughuli zinazofanywa na Mamlaka
KEMI (Swedish chemical agency) kutoka Sweden ambao pia ni washirika wa Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu (TPHPA) kwa muongo mmoja sasa wametembelea ofisi za Mamlaka kwa nia ya kujifunza masuala mbalimbali ya Mamlaka hii haswa katika maswala ya udhibiti wa viuatilifu.
Akizungumza Mwakilishi Kaimu Mkurugenzi Ndg.Osmund Ndomba wakati akiwakaribisha wageni hao ambao wamekuwa wakitekeleza miradi kwa pamoja na TPHPA amesema wamefurahishwa na ujio wao katika ofisi za TPHPA ambapo pamoja na shukran hizo amewashukuru pia KEMI kwa kuwawezesha kupata mafunzo juu ya masuala ya Viuatilifu watumishi takribani 13 wa Mamlaka ambapo ujuzi huo utasaidia Sana katika kuelimisha jamii ya wakulima juu ya matumizi bora ya Viuatilifu kwa ajili ya usalama wa Afya ya mimea,aidha amezungumzia juu ya changamoto ya asilimia kubwa ya wakulima kutojua taratibu mbalimbali zinazotakiwa kufuata katika kufanya biashara za mazao kimataifa ambapo Mamlaka imekuwa ikifanya juhudi Kuwaelimisha kwa kutoa elimu kupitia njia mbalimbali. Akimalizia mazungumzo hayo amesema Mamlaka ipo tayari kutoa ushirikiano na kuwaunga mkono KEMI hivyo wasisite kuleta mezani jambo lolote litakalohitaji usaidizi wa TPHPA.
Sambamba na hilo wageni hao wamepata fursa ya kujua Muundo wa Utumishi katika Mamlaka uliowasilishwa na Kaimu Afisa utumishi Mkuu Bi.Matiku Maiseli aidha taarifa juu ya vyanzo mbalimbali vya mapato vya Mamlaka kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Fedha ndg. Costa Haule .Taarifa ya shughuli mbalimbali za Mamlaka ikiwepo historia ya TPHPA iliwasilishwa na Mr.Raphael Mwezi ambae pia ni Msimamizi wa miradi inayotekelezwa kwa pamoja kati ya KEMI na TPHPA.
Katika kukamilisha ziara hiyo wageni hao wametembelea Idara mbalimbali za Mamlaka ikiwepo Maabara kubwa iliyopo katika ofisi hizo.
Akishukuru mwishoni kiongozi wa KEMI ambae ni Meneja wa Mradi Bi Zoia Faraj amesema wanashukuru kwa mapokezi ya wenyeji wao na ushirikiano mkubwa ambao wamekuwa wakiwapatia katika kutekeleza malengo ya pamoja kama washirika katika kutekeleza miradi, pia ametoa zawadi ya kumbukumbu ya urafiki wao na Mamlaka iliyopokelewa na Kaimu Mkurugenzi Dkt Osmund Ndomba.
Comments
Post a Comment