WATAALAM TPHPA WATAKIWA KUTUMIA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA KONGWE MWITU(SANSEVIERIA) KUPATA TAALUMA NA MBINU ZA UTAFITI WA MMEA HUO
Hayo yamejiri katika kongamano la Kimataifa la SANSEVERIA linalofanyika katika ukumbi wa TPHPA ambapo Mgeni rasmi Dkt.Sospeter Kabululu akimuwakilisha Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka Prof.Joseph Ndunguru amewata wataalam wanaoshiriki kutumia fursa hiyo kujifunza Kwa umakini mbinu mbalimbali zinazotumika katika kutafiti mmea wa Kongwemwitu ambao una maajabu mengi na faida kubwa kwa binadamu na mustakabali wa dunia kwa ujumla.
Akiongea mara baada ya kufungua Kongamano hilo amesema mkutano huu umekusanya Watafiti mbalimbali kutoka ujerumani,ufaransa,Uganda,Kenya, Zanzibar n.k ambapo kwa pamoja wanajadili kuhusu mmea huu wa Kongwemwitu ( Sansevieria) na kuona ni namna gani mikakati ifanyike katika kuhifadhi mmea huu wa kipekee ambao uko katika aina tofauti zaidi ya Mia moja usipotee katika uso wa dunia kutokana na shughuli za binadamu.
"Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu moja ya jukumu letu ni kuhifadhi mimea nasi tunabeba jukumu kuhakikisha mmea huu haupotei na dunia izidi kupata faida zake ,tutaunga mkono mikakati ya uhifadhi na utafiti zaidi wa mmea huu itakayojadiliwa katika kongamano hili ambapo kwa pamoja TPHPA na taasisi ya Tanzania Sanseveria Foundation tutashirikiana katika nyanja tofauti tofauti kuona uhifadhi wa mmea huu unafanikiwa na watanzania waweze kunufaika nao"alisema Dkt.Kabululu.
Akitaja faida mbalimbali za mmea huu Dkt.Neduvoto Maollel ambae ni msimamizi wa Kitengo cha National Herbarium of Tanzania amesema mmea huu unafaida nyingi na tafiti bado zinaendelea kufanyika kujua zaidi baadhi ya faida hizo ni hutumika kama chakula cha wanyama lakini pia ni mmea ambao unastahimili ukame huweza kustawi mahala popote bila masharti mengi,pia utafiti unaonyesha Mmea huu huweza kutumika kama dawa na hata nyuzi zake huweza kutumika kutengeneza nguo.
Kongamano hili la kimataifa lililoandaliwa kwa pamoja kati ya Taasisi ya Tanzania Sanseveria Foundation na TPHPA kupitia Kitengo cha NHT (National Herbarium of Tanzania) ni la siku 6 ambapo wataalam hao watafiti kutoka mataifa mbalimbali watapata nafasi kutembelea maeneo mbalimbali yanayopatikana mmea huu Kwa upande wa Arusha,lakini pia watapata fursa ya kujionea Maabara kubwa ya TPHPA inavyofanya kazi
Comments
Post a Comment