Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mhe. Janeth Mayanja aipongeza FAO na TPHPA


Pichani; Bi Gress Matiku ambaye ni Mtaalamu wa kudhibiti visumbufu vya Mlipuko kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara Mhe. Janeth Mayanja Mashine ya kupandiia (Planter) Leo Disemba 2. 2023 Wilaya ya Hanang 

Pichani Bi Gress Matiku ambaye ni Mtaalamu wa kudhibiti Visumbufu vya Mlipuko kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) akitoa maelezo ya matumizi ya mtego wa kukamata Viwavijeshi kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara Mhe. Janeth Mayanja 










Na Innocent Natai

Kuelekea msimu mpya wa Kilimo Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara Mhe. Janeth Mayanja amelipongeza Shirika la Chakula na kilimo la umoja wa mataifa (FAO) na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kwa ushirikiano walioufanya na kuwezesha kutoa elimu ya namna ya kudhibiti Visumbufu vya Mimea aina ya Viwavijeshi kwa wakulima Mfano na kutoa Vifaa vya Kilimo na Pembejeo za Kilimo ili kuwawezesha kujikwamua katika kilimo na kupunguza madhara yatokanayo na vifumbufu aina ya Viwavijeshi

Mhe. Mayanja Ameyasema hayo leo Disemba 2. 2023 wakati wa hafla fupi iliyofanyika Katika Mji wa Kateshi Wilayani hapo ya kufunga Mafunzo na kugawa Vifaa na Pembejeo za Kilimo zilizotolewa na Shirika la Chakula na kilimo la umoja wa mataifa (FAO) ambapo amesema kuwa vifaa na Elimu iliyotolewa itawezesha wakulima hao kuepukana na Matumizi makubwa ya Gharama wakati wa uzalishaji kwani wakulima hao wamekuwa wakitumia muda mrefu na gharama wakati wa kupambana na visumbufu kitendo kinachowafanya kupata mazao kidogo

Aidha amelishukuru Shirika hilo na TPHPA kwa Msaada huo huku akisema wamekuja muda muafaka kwani ni msimu ambao wakulima hao wanaelekea kwenye uzalishaji,pia amewataka kuongeza wigo wa elimu na msaada kwani Wilaya hiyo ni wazalishaji wakubwa wa mazao nchini hivyo wanahitaji elimu ya kutosha na mbinu bora za kuzalisha 

Akizungumza na Wakulima hao waliopata vifaa hivyo amewataka kuvitumia kwa tija na elimu waliyoipata  kusambaza kwa wakulima wengine ili kwa Pamoja uzalishaji ukaongezeke na pato la kila mmoja katika jamii likakuwe.

Akizungumza mbele ya Mkuu huyo wa Wilaya  Bi Gress Matiku ambaye ni Mtaalamu wa kudhibiti visumbufu vya Mlipuko kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) amesema kuwa mafunzo hayo yamejumuisha wakulima Ishirini na Tano (25) na Maafisa Ugani kutoka Kata mbalimbali za Wilaya hiyo na dhumuni la mafunzo hayo ilikuwa ni kutoa elimu ya udhibiti Shirikishi ya kudhibiti Viwavijeshi Vamizi na kupitia mafunzo hayo wakulima hao wamefanikiwa kujifunza kwa Vitendo mbinu mbalimbali za kumdhibiti Viwavijeshi Vamizi.

Akizungumzia vifaa na pembejeo walizopewa wakulima hao Bi Rose Makange ambaye ni Afisa Kilimo Kata ya Dumbeta amesema kuwa Wamepokea Mashine za Kupandia (Planters),Mitego ya kukamata Madume ya Viwavijeshi, Mabuti, Mask, Miwani Maalumu, Mabomba(Vinyunyizi),Viuatilifu vya Kibaiolojia, Mavazi kinga, Kilo 60 za mbegu, Mbolea ya Kupandia na Kukuzia na vyote vimegawanywa kwa Wakulima hao Mfano.

Kwa upande wao Bi. Elizerbeth Stephano na Bwana Nicholous Leonard amabo ni Wakulima Mfano waliopatiwa mafunzo na Vifaa hivyo wametoa shukrani kwa Shirika la Chakula na kilimo la umoja wa mataifa (FAO) na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kwa elimu na Vifaa kwani vitakwenda kuwasaidia katika shughuli zao za uzalishaji, huku wakiahidi kuvitumia vizuri na kusambaza elimu waliyoipata kwa wakulima wenzao.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu