TPHPA yapiga hatua utekelezaji wa Agizo la Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Leo Januari 25, 2023 Dkt. Osmund Ndomba Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) ameshiriki zoezi la Wakuu wa Taasisi za Umma zilizopo Mkoani Arusha na Halmashauri za Mkoani hapo la Utiaji Sahihi wa Mkataba wa Mfumo mpya wa Usimamizi na Utendaji kazi katika utumishi wa Umma PEPMIS (Public Employee Performance Management Information Sysytem) na Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji kazi katika ngazi ya Taasisi PIPMIS (Public Institutions Performance Management Information System) hii ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anayelenga kuimarisha mifumo ya uwajibikaji inayowezesha viongozi na watumishi wa umma kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wakati na mahali popote. Akizungumza Wakati wa Akifungua Hafla hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Ndg. Missaile Musa amesema kuwa Mfumo wa Usimamizi na Utendaji kazi katika utumishi wa Umma PEPMIS (Public Employee Performance Management Information Sysytem) u...