WAKAGUZI WA VIUATILIFU NA WATUMISHI WA TPHPA WAONYWA KUTOJIHUSISHA NA BIASHARA YA KUUZA VIUATILIFU
Hayo yamejiri katika mafunzo yanayotolewa na FAO Kwa udhamini wa Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na TPHPA yanayoendelea jijini Moshi kwa Wakaguzi wa Viuatilifu kutoka Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA).
Akizungumza Afisa Sheria Mwandamizi wa Kitengo cha Sheria - TPHPA bi.Elizabeth Swai amefafanua vifungu mbalimbali vilivyopo chini ya Sheria ya Mimea Na.4 ya 2020.
Akifafanua kifungu cha 12 na 38 (b) alisema, vinapiga marufuku Wakaguzi wa Viuatilifu na watumishi wa TPHPA kujihusisha na biashara ya viuatilifu,akiongelea adhabu iwapo mtumishi atabainika na kosa hilo amesema atashtakiwa mahakamani na kuhukumiwa kwenda jela au faini ama vyote kwa pamoja .Hivyo amewataka kuzingatia masharti hayo ili kuepuka kuingia matatani.
Pamoja na vifungu hivyo vilevile ameelezea kuhusu Viuatilifu na vinyunyizi vinavyoingizwa nchini ni lazima viwe vimesajiliwa na kupata vibali ,pia wafanya biashara wa viuatilifu lazima wawe wamepata mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viutilifu kutoka TPHPA pamoja na kuwa na vibali vya kufanya biashara husika.Vilevile amesisitiza ni kinyume na Sheria kujihusisha na viuatilifu ambavyo ni feki, vilivyoisha muda wa matumizi na visivyokuwa na ubora unaotakiwa na ikibainika utaratibu umekiukwa muhusika atatakiwa kushtakiwa mahakamani na adhabu stahiki kutolewa.
Hivyo Wakaguzi wamesisitizwa kufanya ukaguzi kwa makini na uaminifu wakizingatia Sheria na kanuni zake zinavyotaka.
Comments
Post a Comment