TPHPA yapiga hatua utekelezaji wa Agizo la Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan









 Leo Januari 25, 2023  Dkt. Osmund Ndomba Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) ameshiriki zoezi la Wakuu wa Taasisi za Umma zilizopo Mkoani Arusha na Halmashauri za Mkoani hapo la Utiaji Sahihi wa Mkataba wa Mfumo mpya wa Usimamizi na Utendaji kazi katika utumishi wa Umma PEPMIS (Public Employee Performance Management Information Sysytem) na Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji kazi katika ngazi ya Taasisi PIPMIS (Public Institutions Performance Management Information System) hii ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anayelenga kuimarisha mifumo ya uwajibikaji inayowezesha viongozi na watumishi wa umma kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wakati na mahali popote.


Akizungumza Wakati wa Akifungua Hafla hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Ndg. Missaile Musa amesema kuwa Mfumo wa Usimamizi na Utendaji kazi katika utumishi wa Umma PEPMIS (Public Employee Performance Management Information Sysytem) utasaidia kuongeza uwajibikaji kwa watumishi wa Umma

Aidha Akizungumzia Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji kazi katika ngazi ya Taasisi Public Institutions Performance Management Information System (PIPMIS) amesema kuwa Mfumo huu ni makubaliano ya kimaandishi kati ya Serikali na Taasisi ya Umma kuhusu malengo ambayo Taasisi husika itayatekeleza katika kipindi cha mwaka mmoja. 


Makubaliano hayo yatakuwa kati ya viongozi wakuu wa Taasisi na Viongozi wao wanaowasimamia katika masuala ya kisera na utendaji wa kila siku. Malengo yaliyomo ndani ya mikataba yatakuwa na vigezo, shabaha na viashiria vitakavyotumika katika utendaji wa taasisi kila mwaka. Utekelezaji wa Mfumo wa Huu wa PIPMIS utaongeza uwajibikaji katika utekelezaji wa sera, mikakati na vipaumbele vya taasisi, sekta na taifa kwa ujumla; kuimarisha utamaduni unaojali matokeo; na kuleta matumizi bora ya rasilimali za umma. Manufaa haya yatatokana na kuwepo kwa vigezo na viashiria vya kupima utendaji wa taasisi katika maeneo hayo 

Katika Mkoa wa Arusha Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imekuwa miongoni Mwa Taasisi Kumi na Tisa 19 zilizokamilisha hatua awali na kufanikiwa kwa Mkuu wa Taasisi kusaini Mkataba huo.

Katika hafla hiyo Dkt. Osmund Ndomba aliambatana na Kaimu Mkuu wa kitengo cha utawala na usimamizi wa rasilimali watu Bi. Matika Maiseli na Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mipango,ufuatiliaji na Tathimini wa Mamlaka hiyo Bwana Mathias Shindika.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu