Mafunzo ya Siku Tano (5) kwa Wakaguzi wa Viuatilifu yahitimishwa, Prof. Ndunguru azungumza na Wahitimu
![]() |
Leo Januari 12, 2024 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania Prof. Joseph Ndunguru ameshirikia katika hafla ya kufunga Mafunzo ya Wakaguzi 32 Wa viuatilifu yaliyoendeshwa Mkoani Kilimanjaro Kwa Siku Tano (5) kwa msaada kutoka Umoja wa Ulaya (European Union)kupitia mradi unaofadhiliwa na ACP MEAs3,Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Kwa kushirikiana na TPHPA
Yakiwa na Lengo la Kuwajengea uwezo wa Kukagua biashara za Viuatilifu ili kusaidia uzalishaji salama wa chakula na ulinzi wa afya ya binadamu na mazingira
Prof. Ndunguru Akibainisha faida ya mafunzo hayo amesema kuwa wataalam hao wanajengewa uwezo ili waweze kufanya majukumu yao ya ukaguzi kwa weledi jambo ambalo litapelekea kulinda afya ya binadamu,mimea na mazingira.
Pamoja na hayo mafunzo yatapelekea kuongeza tija katika uzalishaji kwani ukaguzi utakapofanyika kitaalam na kuzuia yale yote ambayo yangepelekea kuharibu uzalishaji matokeo yake ni kuongezeka tija katika mazao ambayo itapelekea uboreshwaji wa masoko ya mazao kwa kiwango kinachohitajika hata kwa masoko ya kimataifa,
Akitoa wito kwa washiriki Prof.Ndunguru amewataka kuzingatia maelekezo wanayofundishwa ili malengo yanayotarajiwa yakafikiwe,Aidha mafunzo Hayo yamefungwa na Ndug. Alphonce Mwiru ambaye ni Afisa kutoka Idara ya Maendeleo ya Mazao Wizara ya Kilimo akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo
Comments
Post a Comment