TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO









Hayo yamejiri  13/8/2024 katika kituo cha  kudhibiti visumbufu vya mimea kibiolojia ambapo kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mh. Gerald Mweli. 

Akiongea wakati wa kukabidhi Maabara hiyo kwa TPHPA mara  baada ya yeye kukabidhiwa  kutoka kwa Msimamizi wa Mradi TANIPAC  Bwana Clepin Josephat  Mh. Mweli amewataka TPHPA kulinda na kulitunza jengo hilo lakini pia kutokana na malengo  ya ujenzi wa Maabara hiyo matokeo yaonekane na hatimae kuongeza uchumi wa nchi kutokana na kukua kwa biashara ya mazao."Tunatarajia sasa Maabara hii ilikalete matokeo kulingana na malengo ,sisi kama wizara tumefanya sehemu yetu nanyi pia mfanye aidha msisite pale mtakapohitaji ushauri au msaada wowote tuko pamoja nanyi tutafanya kazi kama timu" alisema  Mh. Mweli.

Nae Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa TPHPA Prof.Temu  ameishukuru serikali kwa   kuwezesha kupatikana kwa Maabara hiyo kupitia Mradi wa TANIPAC ambapo amesema Bodi itahakikisha  Maabara hiyo inaleta tija na matokeo mazuri kama ilivyokusudiwa.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea Tanzania Prof.Joseph Ndunguru ameishukuru serikalii kwa kuwajengea Maabara hii ya kisasa kwani itasaidia katika kurahisisha  uchunguzi wa usalama wa chakula,uchunguzi wa mgonjwa ya mimea pamoja

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu