MAFUNZO YA MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA VIUATILIFU YAANZA RASMI IFAKARA

 








Febuari 12, 2024 Mratibu wa mafunzo Ndg. Jumanne Musalama amefungua mafunzo ya matumizi sahihi ya Viuatilifu yanayo tolewa na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kwa wafanya biashara na wakulima yenye lengo la kutoa elimu ya matumizi sahihi ya viuatilifu ili kuepuka madhara kwa binadamu na mazingira yanayotokana na matumizi yasiyo sahihi.


Aidha akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Ndg. Jumanne alieleza faida na madhumuni ya mafunzo hayo hususani kwa wakulima na wafanya biashara  katika kutambua na kutumia viuatilifu kwa usahihi. Ambapo amesema yatasaidia wakulima na wafanya biashara kupata elimu juu ya njia sahihi za  matumizi bora ya Viuatilifu kwani matumizi bora ya viuawatilifu ni muhimu,pamoja na kupelekea mimea kuwa na afya na kuepuka athari mbalimbali



Pia inasaidia kufungua masoko ya ndani na nje ya nchi kwa bidhaa zetu bora na kupelekea ongezeko la kipato kwa wakulima wenyewe na pia kwa taifa letu kwa ujumla kwani matumizi sahihi ya viuatilifu yatasaidia kupunguza kwa ukubwa uwezekano wa kuwepo kwa mabaki ya sumu katika mazao yanayotarajiwa kuuzwa nje ya nchi nakupelekea kukidhi vigezo vilivyo wekwa kimataifa 

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu