Menejimenti ya TPHPA yatembelea vituo vya Ukaguzi Dar Es Salaam, Dkt. Osmund Ndomba aongoza
Na Innocent Natai TPHPA
Febuari 10, 2024 Dkt. Osmund Ndomba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru ameongoza wajumbe wa menejimenti ya Mamlaka hiyo kutembelea vituo ya ukaguzi vya TPHPA, Bandari ya Dar Es Salaam,Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar Es Salaam na Kituo cha Kitaifa cha Kudhibiti visumbufu kwa njia ya kibiolojia ziara hiyo ikilenga kuhimiza utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka na serikali kwa watumishi waliopo katika vituo hivyo
Ziara hiyo imefanyika baada ya kuhitimishwa kwa Mafunzo ya Uongozi kwa wajumbe hao ya siku Moja yaliyoendeshwa na wakufunzi kutoka Taasisi ya UONGOZI
Comments
Post a Comment