Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Prof. Ndunguru aendelea kutekeleza kwa Vitendo Maagizo ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Febuari 7, 2024 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru ameunga mkono agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati akipanda mti aina ya Muembe Pembeni (Mangifera indica) katika eneo la Donge Muwanda, Zanzibar wakati wa kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa tarehe 27 Januari, 2024 ambapo aliwataka viongozi na watanzania kuhamasishana kupanda miti kwaajili ya kutuna mazingira
Hivyo Prof. Joseph Ndunguru baada ya kufungua Mafunzo ya siku moja ya Uongozi kwa menejimenti ya Mamlaka hiyo yaliyoendeshwa na wakufunzi kutoka Taasisi ya UONGOZI, amepanda Muembe katika Ofisi za Mamlaka hiyo kanda ya Mashariki Kurasini Mkoani Dar Es Salaam huku akiwataka washiriki wa Mafunzo hayo kuunga mkono kwa kupanda miti katika maeneo yao
Prof. Ndunguru amesema mufunzo hayo ya viongozi yamelenga kuwajengea uwezo katika uongozi,maadili na kujenga ushirikiano
Kwa Upande wake Kaimu Meneja wa kanda ya Mashariki Dkt. Mahamudu Sasamalo amesema katika kutekeleza adhima ya Mamlaka na Serikali ya kutunza mazingira kwa kupanda miti kanda hiyo imepanga kupanda miti Shule ya Msingi Kiungani miti Kumi na Tano (15), Shule ya Msingi Minazini miti Kumi na Tano (15), Shule ya Sekondari Diplomasia miti Kumi na Tano (15) na Shule ya Sekondari Uhamiaji miti Kumi na Tano (15) hivyo kufikisha jumla ya miti 60
Comments
Post a Comment