TPHPA yawajengea uwezo wa Matumizi sahihi na Salama ya Viuatilifu wakulima wa Mazao ya Viungo na Mpunga Mkoani Morogoro




Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kupitia Kitengo cha Usimamizi wa Teknolojia na Vinyunyizi vya Viuatilifu (PAT) imeto mafunzo ya Matumizi Sahihi na Salama ya Viuatilifu kwa Wakulima wa Mazao ya Viungo na Mpunga katika Wilaya za Mvomero na Morogoro vijijini zote zikipatikana katika Mkoa wa Morogoro.

Machi 18,2024 Akizungumza katika Mafunzo hayo Dkt. Magreth Mwangi amesema kuwa mafunzo hayo yamefanyika katika Kata Tano (5) katika Wilaya hizo ambapo mafunzo hayo yalilenga kuwezesha wakulima kulima kilimo salama na chenye tija kwa kupulizia Viuatilifu wakiwa wamejikinga na kuhifadhi maeneo salama vifungashio vya Viuatilifu vilivyotumika.

Kwa upande wao Wakulima wa Kata hizo waliopata mafunzo hayo wamewashukuru wataalamu hao Kwani kabla ya Mafunzo hayo wameeleza kuwa walikuwa wakitumia Viuatilifu Vingi bila kufuata taratibu hivyo kupata hasara za mazao na kifedha,pia wamesema walikuwa wakiathirika na viuatilifu bila wao kujua kutokana na tabia ya kutokuhifadhi vizuri Vifungashio vya Viuatilifu baada ya Matumizi

Hivyo wameahidi kutumia vyema elimu hiyo kwaajili ya Usalama wao na kuzalisha mazao yatakayopata masoko ndani na nje ya Nchi kwa kusafirisha mazao yasiyo na Masalia makubwa ya Viuatilifu.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu