WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI TPHPA WATEMBELEA OFISI ZA TPHPA NAMANGA,WAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU

 







Wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Afya ya mimea na Viuatilifu  wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof.Andrew Temu 19 Machi 2024 wametembelea ofisi za Mamlaka  zilizopo mpakani mwa Kenya na Tanzania Namanga pamoja na Kituo cha kijasusi cha ukusanyaji wa taarifa za masoko nje ya nchi,lengo likiwa ni kujionea shughuli na changamoto mbalimbali kwa ajili ya kupata ufumbuzi.


Akiongea mara baada ya ukaguzi sehemu mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka kama vile eneo la ukaguzi,maabara Prof.Andrew Temu amewapongeza kwa namna wanavyofanya kazi kwa kushirikiana na taasisi zingine 18 za serikali zilizopo mpakani hapo lengo likiwa ni kufikia matakwa ya serikali,"Kwa ushirikiano huu niliouona hapa naahidi kuwa balozi wenu nitalisemea hili kila mahali nitakapokwenda aidha nawapongeza sana mamlaka kwa jinsi mnavyochapa kazi katika kuhakikisha sheria zinafuatwa na kuondoa ukiukwaji unaoweza kuleta madhara kwa afya zetu na uchumi wa Tanzania,mna wajibu mkubwa wa kuhakikisha mazao yapo salama kuanzia katika uzalishaji mpaka usafirishaji ili kutekeleza haya ushirikiano na taasisi zingine ni muhimu.


Vilevile Wajumbe wa Bodi wamepata nafasi ya kujionea jinsi Kituo cha intelijensia cha ukusanyaji wa taarifa za  masoko duniani kilichopo katika ofisi za Mamlaka Makao Makuu Ngaramtoni kinavyofanya kazi katika sehemu zake zote ikiwepo sehemu maalum ya kuangalia masoko ya Ulaya yanahitaji nini ili kumsaidia mkulima kupata taarifa lakini pia uchambuzi wa tishio la visumbufu kutoka nchi za nje na namna bora ya udhibiti mara baada ya kugundua uwepo wa Visumbufu.


Akipongeza mara baada ya kushuhudia shughuli zinazofanywa na Kituo hicho Prof.Temu ameishauri Mamlaka kuwa na watoa huduma wenye  uhakika hasa katika masuala ya mtandao lakini pia kutoa mafunzo mara kwa mara kwa watumishi wa kituo hicho ili kuongeza ufanisi .


Nae Mkurugenzi wa Mamlaka Prof.Joseph Ndunguru akiongelea kuhusu mipango ya  uboreshaji wa huduma ya kudhibiti visumbufu kupitia huduma ya kituo hicho amesema tayari wamepatikana Wafadhili kutoka Marekani ambao watasaidia kutoa fedha katika kudhibiti Visumbufu ili kuongeza tija kwa wakulima.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu