Prof. Joseph Ndunguru afika Maonesho ya Saba Saba, Atuma ujumbe kwa Wadau

 










Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru ametoa rai kwa wadau mbalimbali wa Kilimo nchini kutembelea katika katika maonesho ya 48 ya kibiashara ya kimataifa (Saba Saba) Dar es salaam hususani katika banda la TPHPA ili kuweza kupata Elimu na Huduma Mbalimbali


Ameyasema hayo leo Julai 10, 2024 wakati alipotembelea katika maonesho hayo katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere  jijini Dar es salaam ambapo ameeleza kuwa TPHPA imeendelea kutoa elimu na huduma kwa wadau nchini ili kuhakikisha wanafikia adha ya Serikali ya kumkomboa Mkulima 


"Wadau tembeleeni katika banda letu hapa Tent la Katavi mtapata kufahamu masuala mengi kuhusiana taratibu mbalimbali za kufanya biashara za mazao na viuatilifu." amesema Prof. Ndunguru


Katika ziara hiyo, Prof.Ndunguru alipata pia nafasi ya kutembelea katika mabanda mengine ya Taasisi na bodi zilizopo chini ya Wizara ya Kilimo


Aidha Maonesho haya yalianza Juni 28,2024  na yanayotarajiwa kuhitimishwa Julai 13.2024 Huku yakiongozwa na kauli mbiu isemayo "Tanzania mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji"

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu