TPHPA Kwa kushirikiana na taasisi zingine yaanza Mikakati kupunguza Vifo vinavyotokana na Viuatilifu
















Katika warsha iliyohudhuriwa na washiriki kutoka Mamlaka na Taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali iliyofanyika tarehe 13 mpaka 14 Agosti 2024, Hapa Mkoani Arusha washiriki waliweza kujadiliana na kupata mafunzo ya kutumia programu iitwayo “KoboCollection

Programu hii yenye kufanya kazi maalumu ya kuhifadhi taarifa za Idadi ya Vifo vilivyotokana na kujiua kwa kutumia Viuatilifu ambapo taarifa hizo zitatumika na Mamlaka za Usalama na Afya ya Mimea kufahamu ni sumu au viuatilifu gani vinatumiwa na watu wanaotaka kujiua, umri wao, mahala pa tukio na taarifa zingine muhimu.

Wawakilishi kutoka vyombo vya Usalama, Wizara ya Afya, Kilimo na Mamlaka za Mazingira waliongozwa na Mwezeshaji kutoka Shirika lisilo la Kiserikali kutoka Kenya (CEJAD) Ndg. Fredrick Otieno ambapo alisema mradi huo utasaidia kuondoa changamoto hiyo ikiwa vyombo husika vitatoa ushirikiano kwani vifo vya kujiua kwa kutumia viuatilifu vinazidi kuongezeka.

Pia aliongeza kwa kuelezea baadhi ya njia zitakazotumika kutekeleza mpango huo ikiwa ni kuzuia sumu zitakazobainika kutumiwa sana na watuhumiwa na pia kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi na salama ya viuatilifu.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu