Jumla ya washiriki 82 wamehitimu mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu Kanda ya Nyanda za juu Kusini.
Washiriki hao wameishukuru Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania(TPHPA), kwa kuwaongezea uelewa zaidi na wameahidi kuwa watahakikisha wanaenda kuyafanyia kazi mafunzo hayo.
Akifunga mafunzo hayo Afisa Kilimo Mkoa wa Njombe ndug. Wilson Joel amesema, kipimo kwa washiriki baada ya mafunzo hayo ni namna watavyoweza kupunguza malalamiko ya wakulima na kuthibiti visumbufu.
Aidha, amewasisitiza wafanyabiashara wa viuatilifu kuajiri watu waliopatiwa mafunzo hayo ili waweze kutoa huduma iliyosahihi.
Bwana Wilson amesema, mafunzo hayo yanalenga moja kwa moja afya za watu hivyo washiriki hao wakatekeleze yote waliyofundishwa.
Mafunzo ya matumizi sahihi na salama ya Viuatilifu Kanda ya Nyanda za juu kusini yamefungwa rasmi Septemba 14 Makambako Mkoani Njombe
Comments
Post a Comment