Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA Afungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi - Mwanza






                                          






















TPHPA- MWANZA

Leo, Septemba 10, 2024, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Prof. Joseph Ndunguru, amefungua rasmi kikao cha siku moja cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Jijini Mwanza


Katika hafla hiyo, Prof. Ndunguru alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya wafanyakazi na uongozi ili kuimarisha utendaji na kuongeza ufanisi katika sekta ya afya ya mimea na viuatilifu. Alibainisha kuwa kikao hiki ni fursa muhimu kwa wafanyakazi kutoa maoni, kujadili changamoto, na kupanga mikakati ya kuboresha huduma na mazingira ya kazi.


Kikao hicho kilihudhuriwa na Menejimenti, Wakuu wa Vitengo na Kanda, wawakilishi kutoka Vitengo mbalimbali vya Mamlaka, pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka. Wakati wa kikao, masuala kadhaa muhimu yaliyojadiliwa ni pamoja na mipango ya maendeleo, mbinu za kuongeza tija, na mikakati ya kuhakikisha utekelezaji wa sheria na kanuni katika sekta ya Kilimo.

Kikao hicho kimekuwa hatua muhimu katika kuimarisha mawasiliano na uhusiano wa kazi kati ya viongozi na wafanyakazi, na kinatarajiwa kuchangia pakubwa katika kuboresha utendaji wa TPHPA katika siku zijazo.

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu