TPHPA yazidi kuwanoa Maafisa wake katika Matumzi ya TEHAMA, Dkt. Oshingi Shilla Afungua Mafunzo ya Siku Mbili













TPHPA - MWANZA

Leo, Septemba 12, 2024, katika Ukumbi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Buzuruga, Jijini Mwanza, Dkt. Oshingi Shilla, akimwakilisha  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), ameongoza ufunguzi wa mafunzo muhimu ya siku mbili kuhusu Mfumo wa e-board. 


Mfumo wa e-board ni teknolojia ya kisasa iliyokusudia kuboresha na kuharakisha uratibu wa shughuli za uandaaji vikao vya bodi na menejimenti katika Taasisi na Mamlaka za Umma. Mfumo huu unasaidia katika kuandaa yatokanayo kwenye kikao, kupiga kura, na kutengeneza ripoti za utendaji kazi katika vipindi mbalimbali vya mwaka. 


Katika hotuba yake, Dkt. Shilla alisisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika kuongeza ufanisi na uwazi katika usimamizi wa vikao. Alieleza kuwa Mfumo wa e-board unalenga kuimarisha usimamizi wa shughuli za bodi na menejimenti kwa kuzingatia ufanisi na uharaka, huku ukifanikisha uratibu mzuri na uwezeshaji wa kazi kwa wahusika wote.


Mafunzo haya yanatolewa na wataalamu wa TEHAMA kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao e-GA. Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wahusika wa kuandaa vikao, hasa sekretarieti, ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi na kuwawezesha wajumbe wa menejimenti kufanya kazi kwa weledi kupitia matumizi ya teknolojia.


Mfumo wa e-board unachangia kuboresha utaratibu wa kawaida wa uandaaji vikao, na hivyo kuwezesha taasisi kuongeza tija katika shughuli zao. Kwa kupitia teknolojia hii, TPHPA inatarajia kufanikisha usimamizi bora wa vikao vyake, kupunguza mzigo wa kazi, na kupunguza matumizi ya karatasi.


**#TPHPA #eBoard #TMDA #TEHAMA #Mafunzo #UratibuVikao #TeknolojiaKatikaMenejimenti**

Comments

Popular posts from this blog

Ni TPHPA tena! yatwaa tuzo Mshindi wa Kwanza

TPHPA WAKABIDHIWA MAABARA YA KISASA ILIYOGHARIMU BIL.3.8, KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATOA MAAGIZO

Kanda ya Kaskazini yatolewa kimasomaso na TPHPA Mashindano ya SHIMMUTA 2024//Yatwaa Mataji Matatu huku ikiweka rekodi Maalumu