LICHA YA KUWA PANYA NI KITOWEO MAARUFU CHAKWALE, WAKULIMA WAELIMISHWA KUWADHIBITI KWA SUMU KUEPUKA MADHARA
TPHPA - Gairo
Maonesho ya Samia Kilimo Biashara Expo 2024 msimu wa 3 Gairo yamewafikia wananchi wa kijiji cha Chakwale ambapo Wataalam wa TPHPA waliopo katika maonesho hayo wamewapa mafunzo wananchi na Wakulima namna ya kutumia Viuatilifu na jinsi ya kutumia mitego ya kutegea panya mashambani na namna bora ya kuwadhibiti kwa Sumu majumbani.
Aidha wametahadharishwa kutowatumia kama kitoweo Panya ambao watakuwa wameuliwa kwa sumu kwani watawaletea madhara ya kiafya.
Akizungumza Mwenyekiti wa CCM GAIRO Mhe. Danistani Daudi Mwendi amewataka wananchi hao kujitokeza kwa wingi kesho 12/10/2024 katika kufunga maonesho haya kijijini Rubeho.
Sambamba na ilo kawasisitiza wananchi wakajiandikishe katika daftari la wapiga kura na wanaotaka kugombea nafasi za uongozi wakachukue fomu ili kugombea nafasi mbalimbali kwani ni haki yao.
Comments
Post a Comment