Maandalizi ya Timu za TPHPA kwaajili ya Mashindano ya SHIMMUTA 2024 yaanza kuwatisha Timu Pinzani
![]() |
TPHPA - Arusha
Timu za wafanyakazi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) zinaendelea na mazoezi kwa ajili ya mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi, na Makampuni Binafsi (SHIMMUTA) 2024, yatakayofanyika mwezi Novemba mwaka huu Mkoani Tanga.
Katika maandalizi haya, timu ya mpira wa miguu ya wanaume imeanza kwa kucheza michezo miwili katika Mashindano ya SHIMMUTA northern zone, Mchezo wa kwanza ulifanyika tarehe 5 Oktoba 2024, ambapo walikabiliana na Timu ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) Katika mchezo huo, TPHPA ilikosa goli na kumaliza kwa matokeo ya TPHPA (0) na NCAA (1). Hata hivyo, timu ya wanawake ya TPHPA ya Mpira wa Pete ilipata ushindi mzuri kwa kuibuka na goli 19 dhidi ya 11 dhidi ya Timu ya Wanawake wa Mamlaka hiyo ya Hifadhi ya Ngorongoro
Katika mchezo wa pili, timu ya wanaume ya TPHPA ilicheza dhidi ya Arusha Technical College (ATC) na kufanikiwa kupata ushindi mkubwa wa TPHPA (3) na ATC (0). Ushindi huu unatoa motisha kwa wachezaji na kuimarisha maandalizi yao kuelekea mashindano makubwa yanayokuja.
Michezo mingine inatarajiwa kuendelea katika juma hili, huku timu zote zikiwa na malengo makubwa ya kufanya vizuri katika mashindano ya SHIMMUTA. Timu za TPHPA zinaonyesha ari na juhudi za hali ya juu, na mashabiki wanatarajia kuona matokeo bora kutoka kwa wachezaji wetu.
Tunaendelea kuwapa sapoti wachezaji wetu na tunawatakia kila la heri katika maandalizi yao!
Comments
Post a Comment