MAONESHO YA SAMIA KILIMO BIASHARA EXPO 2024 MSIMU WA 3 GAIRO YAFUNGWA NA MKUU WA MKOA WA MOROGORO,ATEMBELEA BANDA LA TPHPA.
TPHPA- Gairo
Ikiwa ni siku ya 7 na ya mwisho ya maonesho haya ya Samia Kilimo Biashara Expo 2024 msimu wa 3 Gairo katika Kata ya Rubeho kauli mbiu ikiwa “Tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa maendeleo endelevu ya kilimo na mifugo “ Maonesho haya yamefungwa leo tarehe 12/10/2024 na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Adamu Malima Kwa kuwapongeza wadau wote walioshiriki maonesho haya na kuwapongeza wananchi wote walioshiriki na kuwataka kutumia fursa walizokutana nazo na pia kuitumia vyema elimu katika maeneo mbalimbali ili yawe na tija na kufikia malengo.
Akiwa katika banda la TPHPA Mkuu wa Mkoa Mhe. Adamu Malima ameipongeza Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania kwa kutekeleza majukumu yake vyema na kuelimisha wakulima ili kuwawezesha kunufaika na mazao wanayozalisha hata kuifanya serikali kufikia lengo lake ifikapo 2030 .
Akizungumzia uchaguzi wa viongozi wa Mitaa Mh. Malima amewataka wananchi waendelee kujiandikisha katika daftari la kupiga kura na kisha kuitumia haki yao ya kupiga kura na kuwachagua viongozi sahihi kwa maendeleonya nchi yao.
TPHPA ilishiriki kikamilifu katika maonesho haya na kuelimisha umma juu ya majukumu mbalimbali ya Mamlaka lakini pia kuelimisha juu ya taratibu mbalimbali za kufuata katika usafirishaji wa mazao nje ya nchi,usajili wa viuatilifu,vibali vya kufungua biashara za viuatilifu,taratibu za uingizwaji wa viuatilifu nchini nakadharika.
Comments
Post a Comment