NAIBU WAZIRI KILIMO MH.DAVID SILINDE AZIPONGEZA TAASISI NA MAMLAKA ZINAZOSHIRIKI SAMIA KILIMO BIASHARA EXPO
TPHPA - Gairo
Hayo yamejiri leo tarehe 8 oktoba 2024 katika viwanja vya shule ya Msingi Gairo A ambapo Mheshimiwa David Silinde amefungua rasmi maonesho ya Samia Kilimo Biashara Expo 2024 ,ametoa pongezi kwa Taasisi na Mamlaka zilizoshiriki Maonesho hayo kwani wameonyesha kuunga juhudi za Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha Kilimo chenye tija ili kumuinua mkulima na kumletea maendeleo.
Aidha amebainisha kuwa kushiriki katika maonesho haya kuna faida nyingi ikiwepo kujua fursa mbalimbali zinazoweza kuwaletea maendeleo na kukuza uchumi,pia ni fursa nzuri ya kuwakutanisha wakulima na wafugaji jambo ambalo linajenga umoja.
Akizumgumzia fursa za Wakulima kujiongezea mitaji amewasisitizia wajiiunge katika saccos ya wakulima ili kupata mikopo itakayoinua na kuboresha kilimo chao kisha kuwakwamua kiuchumi.
Pamoja na hayo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa viongozi wa Mitaa ili kuwapata viongozi sahihi watakaowatumikia na kuwaletea maendeleo katika maeneo yao. .
Comments
Post a Comment