SAMIA KILIMO BIASHARA EXPO 2024 GAIRO YAKUTANISHA WANANCHI NA WATAALAM TPHPA ,WAPATA ELIMU
Ikiwa ni siku ya pili ya maonesho ya Samia kilimo biashara expo 2024 yanayoendelea hapa Gairo wananchi wameendelea kupata elimu kutoka kwa Wataalam wa TPHPA ikiwepo umuhimu wa kuzingatia matumizi sahihi ya uchaguzi wa mabomba ya unyunyiziaji wa sumu ili kutokomeza Visumbufu katika mimea.
Akijibu swali kutoka kwa Mkulima kuhusu namna Mamlaka inavyohusika katika mchakato wa usafirishaji na uuzaji wa mazao ya Wafanyabiashara nje ya nchi Mtaalamu wa TPHPA ndg.Bilali amesema Mamlaka ina jukumu katika kutoa Cheti cha usafi wa mazao na kuruhusu kusafirishwa nje baada ya taratibu zingine kufuatwa ambapo ukaguzi hufanyika katika mazao ili kuhakikisha usafi wa mazao yanayosafirishwa umezingatiwa na iwapo vigezo vingine vya kimataifa vimefuatwa kikamilifu,hivyo aliwasihi kufuata taratibu ili kuepuka usumbufu.
Pamoja na hayo wananchi na Wakulima wanapata nafasi ya kuijua vizuri Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu kutokana na maelezo na elimu wanazoendelea kupata kutoka kwa wataalam kuhusu majukumu mbalimbali ya Mamlaka hii.
Maonesho haya yenye kauli mbiu ya "Tunza mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa maendeleo ya Kilimo na Mifugo"yanatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 12/10/2024.
Comments
Post a Comment